ZIFAHAMU BAADHI YA AYA ZA QURAAN ZINAZOHIMIZA AMANI NA MATENDO MEMA KWA BINADAMU WOTE
NDUGU wasomaji wangu karibuni katika Makala yetu ya leo ikielezea baadhi ya aya zinazohimiza amani na upendo. Katika Uislamu, Quraan ni maandiko matakatifuambayo yanatoa mafundisho kwa waumini wa dini hiyo, katika maandiko hayo kuna baadhi ya aya ambazo zinatumika katikakusisitiza matendo ya amani kama ilivyo maana ya neno ‘islamu’, ambapo matendo hayo yanapelekea binadamu kuwa na mwisho mwema hapa duniani na akhera.
Vile vile uwepo kwa matendo hayo mema yanayopelekea kuwepo kwa amani na utulivu yatasaidia jamii kupata maendeleo.
Ili kuishi katika matendo hayo mema ni vyema kujifunza elimu ya dini ikiwemo Qur,ani, hadithi na sunna za mtume Muhammad (S.A.W).
Zifuatazo ni baadhi ya aya ambazo zinahimiza amani na matendo ya Amanikatika dini ya kiislamu.
AYA YA 8 katikaSURAT MAIDAH, Aya hii inaeleza kuwa “Enyi waumini simameni imara kwaajili ya Mwenyezi Mungu na mchukue haki ushuhuda.Usiruhusu chuki ya watu ikupeleke kwenye dhulma. Kuwa mwadilifu, huko ndiko karibu na haki. Na mcheni Mwenyezi Mungu .Hakika Mwenyezi Mungu anayo habari za mnayotenda”.Lengo kuu la mafundisho ya aya hii nikutenda haki na kutomtendea mtu mwengine mabayabila kujali dini yake , kabila hata rangi.
Katika SURAT QAAF AYA 45, Aya hii imeeleza kuwa “Sisi tunajua Zaidi wanachosema na wewe Ewe Mtume si wakuwalazimisha kuamini , hivyo wakumbushe kwa quraantu sio kuwalazimisha”, lengo la aya hiikuhimiza matumizi sahihi ya quraani hasa katikakuwalingania watuna kutumianguvuna vitisho kama wanavyofanya wanaharakati.Ayahiiikufuatwaipasavyo itasaidia kuwepo kwa matendo ya amani anautulivu katika jamii.
AYA YA 14katika SURAT JATHIYAH, Aya hii imeeleza kuwa “Sema , Ewe Muhammed , kwa wale walioamini kwamba wawasamehe wale wasiotarajia siku za Mwenyezi Mungu , ili awalipe watu kwa yale waliyokuwa wakiyachuma “ lengo la aya hiini kuwakwa mtu anayekosea haukumiwina binaadamu mwenzie bali Mungu ndio anayetoahukumu na endapo akatokea mtu au kikundi cha watuakahukumu watu wengine atakuwa ameenda kinyume na maamrishio ya Mwenyezi Mungu na Mtume Muhhammed (S.A.W)
Katika SURAT BAQARA AYA AYA 194, Aya hii imeeleza kuwa “kutakuwa na kisasi katika mwezi mtakatifu kwa kosa katika mwezi mtakatifu na ukiukwaji wote utaleta kisasi. Kwa hiyo, mtu akikushambulia, lipiza vivyo hivyo lakini kumbuka Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu yupo pamoja na wacha Mungu”. Lengola ayahii ni kuwakazi ya kuhukumuaachiwe MwenyeziMungu,badala yahukumu hiyo kufanywana binaadamu dhidiya binaadamu wenzao.
AYA 161 katika SURAT AL ANAFAL, Aya hii imeeleza kuwa “ikiwa adui ana mwelekeo wa amani, fanya amani nao . Na mtegemee Mwenyezi Mungu .Hakika yeyepeke yake ndio mwenye kusikia, mjuzi wa yote “ lengo la aya hii ni kusisitiza amani na utulivumiongoni mwa binaadamu wote na hukumu mwenye haki ya kutoa niMungu pekee.
Wito wangukuwa elimu ni (mali , bahari, rasilimali,ufunguo wa maisha , ukombozi , uhai na fumbo laujinga), hivyokuna umuhimu mkubwa kwajamii kupata elimu ili kujikomboa kifikrana kuzuia watu wasiingie katika vitendoviovu katika jamii ambavyo vinaweza kuleta athari kubwa katika jamii.
Hata hivyo kuna umuhimu wa kusoma elimu (elimu ya dini)ilikupata maana sahihi za ayambalimbalihasa zinazohimiza kuwepo kwa amani na utulivu, hali hilo itasaidia kuwepo kwa maendeleo katika jamii na Nchi kwa ujumla. Pia ufahamu wa aya hizo utasaidia kubaini watu ambao wanataka kutumia aya hizo kufanya upotoshaji kwa wengine.
0 Comments